Jumatano, 30 Julai 2014

MSIMAMO WA NDUGU ZITTO KABWE KUHUSU MCHAKATO WA KUANDIKA KATIBA MPYA

Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Mh. Zitto Kabwe

Jana tarehe 29 Julai, 2014 nimefanya mahojiano katika kipindi cha PowerBreakfast kinachorushwa na Clouds FM. Baadhi ya vyombo vya habari vimeandika mahojiano yale. Napenda nitoe ufafanuzi kidogo kuhusu msimamo wangu kuhusu machakato wa katiba.

Kwanza, Mimi sijawahi kuwa UKAWA wala kundi lolote lile katika Bunge Maalumu la Katiba isipokuwa kundi linalotaka maridhiano. Msimamo wangu kuhusu Muungano ni Serikali Zilizoboreshwa (S3z) ili kuwa na Muungano imara usio tegemezi wala egemezi kwa Washirika wake.

Pili, Mimi niliunga mkono 'protest' ya baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kupinga lugha za matusi na lugha za kibaguzi zilizokuwa zinaendelea ndani ya mkutano ule. Vilevile niliunga mkono kwamba Rasimu inayoopaswa kujadiliwa ni Rasimu iliyotokana na Tume ya Marekebisho ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Sinde Warioba. Nasisitiza umuhimu wa kupata Katiba BORA itakayoimarisha DOLA ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Tatu, kwa hali ya sasa kuna mkwamo katika kupatikana kwa katiba Bora. Mkwamo unaotokana na kutokuwepo kwa nia ya dhati ya kupata maridhiano ya pande zinazopingana. UKAWA hawataki mazungumzo na viongozi w Bunge la Katiba badala ya kujenga maridhiano kila siku wanawabeza UKAWA jambo ambalo kamwe haliwezi kujenga mwafaka. Ushauri wangu ni kuhairisha mchakato mzima wa kuandika katiba mpaka mwaka 2016 baada ya uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. Katiba ya sasa ifanyiwe marekebisho machache kama ifuatavyo;

i)Tume ya Uchaguzi ili iwe huru na ionekane kuwa huru, ikiwemo kuwaondoa watumishi wa Halmashauri za Wilaya, Miji na Majiji katika kusimamia uchaguzi.

ii) Kuruhusu mgombea binafsi

iii) Kuondoa Mafuta na Gesi kama Jambo la Muungano ili Zanzibar ianze mara moja kusimamia kwa uhuru utafutaji wa Mafuta katika vitalu vilivyopo upande huo wa Muungano.

Mkutano wa Bunge Maalumu utakaofanyika bila kuwepo maridhiano utakuwa hauna maana yeyote na itakuwa ni sawa na kupoteza muda na fedha za walipa kodi ambazo zingeweza kununua madawa vijijini. Mimi binafsi sitahudhuria mkutano wa Bunge Maalumu kama makundi hasimu hayatakuwa yamefikia maridhiano.

Kabwe Zitto, MB/MBMK

RUMOR HAS IT! HUSSEIN MACHOZI ANACHEPUKA NA SIZE 8


UGANDA: PICHA ZA UTUPU ZA MWANAMUZIKI BRENDA NAMBI ZAVUJA TENA


Mwanamitindo mwanamuziki wa Uganda, Brenda Nambi, anaendelea kupata karaha jinsi gani atasafisha jina lake baada ya picha zake za utupu kusambaa mtandaoni katika hali ambayo hata yeye mwenyewe hakutegemea. 

Hii sio mara ya kwanza kwa Msanii Brenda Nambi kukutwa na mambo ya ajabu kama hayo, wakati flani ilisambaa Sex Tape yake akiwa na Celeb wa Uganda maarufu kama Seya. Hii nayo ilitokea wakati ambapo Brenda alionekana kama kufeli muziki na kuamua kukubali kusainishwa kwenye mtandao wa kingono wa 'Alibhai' kisha kuwa trained jinsi ya kuwananiino wanaume mbele ya camera.

Picha zake za utupu zilizovuja ni hizi...


CHANZO NI MTANDAO WA http://juicyfile.com

Jumanne, 29 Julai 2014

BABA ACHARAZA VIBOKO WALIMU

Kamanda wa Polisi Mkoani Tabora, Suzan Kaganda
Vitendo vya baadhi ya wazazi , kudhalilisha walimu vinaendelea ambapo mzazi mmoja Selemani Juma, amewashambulia walimu wawili kwa viboko.

Amefanya hivyo kupinga mwanawe kurudishwa nyumbani, akashone kaptura. Alifanya hivyo mwishoni mwa wiki iliyopita. Taarifa zinasema Juma alidhalilisha walimu wawili wa Shule ya Msingi Nzogimlole iliyopo wilayani Nzega Mkoani Tabora.

Kwa Mujibu wa Mwalimu Josephat, Mwalimu aliyeshambuliwa (Jina limehifadhiwa), alikuwa akifundisha katika darasa hilo na alipomuona mwanafunzi huyo kavaa kaptura iliyochanika vibaya, kiasi cha sehemu za siri kuonekana, alimrudisha nyumbani kwenda kurekebisha sare yake na ndipo kisanga kikamrudia.

CHANZO: GAZETI HABARI LEO. Imeandikwa na Lucas Raphael, Tabora.

MZEE WA MIAKA 66 ANAYEDAI KUWA YEYE NI YESU KRISTO



Mzee wa miaka 66, m'brazil kwa miaka 35 amekuwa akihubiri Injili - Kwasababu anaamini yeye ni uzao mpya katika pumzi na nafsi ya Kristo.
Anajiita 'INRI'. Inri ni neno la kiyahudi maana yake Yesu wa nazareti mfalme wa wayahudi. Hadi sasa hivi ana mamia ya wafuasi UK, Ufaransa na Britain na baadhi yao wanaishi nae kanisani kwake, nje kidogo ya Brasilia.

Tangu mwaka 1979 amesafiri zaidi ya nchi 27 akihubiri injili ya neno la Mungu, ingawa baadhi ya nchi kama Britain, US, na Venezuela walimfukuza kwasababu ya mafundisho yake yenye utata.

Mwanafunzi wake mdogo kabisa ambae sasa hivi ana miaka 24, alikutana nae akiwa na umri wa miaka 2. Mahubiri yake, uvaaji wake kwa mfano wa Kristo,  maoni yake juu ya ubepari na hata Krismasi kumfanya atiwe kizuizini na polisi zaidi ya mara 40.

SONY WAMELETA SAA ZA MKONONI, ZINA INTERNET, UTAWEZA KUSOMA EMAIL KUPERUZI FACEBOOK NA TWITTER PIA


Product mpya ya Sony ipo sokoni, ni saa za mkononi, zenye uwezo kama smartphone. Mtu anaweza kutumia internet kusoma email, kuperuz facebook na twitter pia. Moja ni sawa na Ksh 19,500/=

IBADA ZA KANISANI KUPITIA APPLICATION MPYA YA iPHONE

Ukrain wameamua kurahisishia watu kuabudu kwa muongozo ule ule unaotolewa na Padre kanisani, kupitia Application mpya ya iPHONE. Wadau wanasema kwamba waligundua kwamba vijana ni wavivu kuhudhuria ibada, kwamba interest yao kubwa wanapenda kukaa kwenye social networks, kwahiyo kupitia computer pia application hiyo itasaidia ibada kuendelea. Kupitia hii Application mtu anaweza kuuliza na hata kuomba msaada kwa padre na akapata majibu.

ONA WALICHOFANYA MASHABIKI WA BEYONCE

Baada ya Nicki Minaj kutangaza kusogeza mbele uzinduzi wa Single yake ya ANACONDA, mashabiki wametoa RMX ya COVER aliyotangulia kutoa Nicki, This time katupiwa Beyonce! Acha kabisa photoshop ni kitu ingine, angalia...
Sasa hiyo ya juu wametengeneza mashabiki wa Beyonce, ila Origina yake kabisa ni hii hapa chini ambayo ametokea Nicki Minaj. 


Ijumaa, 11 Julai 2014

Utaiga watu kuvaa ila kwa Rihanna utazima fegi

Hivi unaikumbuka hii kutoka kwa Rihanna? Kama ulidhani anatafuta kiki, angalia leo alichovaa!





Wakati wewe unajipanga ukitoka upigilie mtoko wa sampuli gani washkaji wakuone umetoka chicha, Rihanna anaingia kwenye rekodi mpya ya kufanya vile akili yake inavyomtuma.

Hivi hii ni dress code gani!


Movie: Mpya kutoka kwa Tom Cruz,The Snap

Mwezi Julai umekua mwezi ambao umeboa sana kwenye suala la muvi sokoni. Kama unapenda muvi utakua umesanuka kuwa muvi ambazo zimekua zikitoka zimekua za kawaida kuliko tulivotaraji.

Mfano wakati ilipotangazwa kutoka Muvi ya 'Transfomers', haikuwa kwenye kiwango ambacho wapenda sinema walitaraji. Mpya kutoka kwa Tom Cruz ni hii inaitwa 'The Snap'

Fuatilia zaidi kupitia hii link: https://www.youtube.com/playlist?list=PLbyV-UUzqn5ntLuFEEgOZlXyRlFC_zUeD

Wale wa Fashion & Beauty kona hii inakuhusu

Huyu sio Lupita Nyong'o ni Herieth Paul! Sasa anafata nyayo za Flaviana Matata & Anisa Mpungwe

Fashion siku hizi imekua dili sana, kama unapenda fashion na ukawa na vigezo vya kutosha mafanikio yakianza kuja hata maisha yako huenda yakabadilika kwa kiwango kikubwa. Mtazame huyu binti wa kitanzania vizuri! 


Ukimtazama utadhania umemuona Lupita Nyong'o lakini sio, alivyo mwembamba, kipimo cha urefu wake na ambavyo rangi ya ngozi yake inavutia ni haki tukisema anawanyemelea akina Flaviana Matata na models wengine waliofanikiwa kimataifa akiwemo Anisa Mpungwe.

Huyu ni Mtanzania na anafanya kazi kama model kutangaza mavazi ya makampuni ikiwemo bidhaa mbalimbali za mashirika binafsi. Angalia mitupio yake alafu acha comment zako kama vipi.

Exclusive: AFRIMA wametangaza nafasi za ushiriki wa wazi


Tuzo za muziki 'AFRIMA' nchini marekani kwa kushirikiana na Umoja wa Africa (Africa Union) wameamua kupanua wigo wao kwa kutangaza nafasi za wazi za ushiriki wa tuzo hizo. 

Lengo kubwa ni kutoa fursa kwa wasanii mbalimbali, kukuza vipaji vya wana-sanaa wa Afrika, kuwapongeza kwa tuzo ili kuutangaza utamaduni wa nchi zao (za Afrika) ambao kirahisi utatambuliwa na dunia.

Wanaoruhusiwa kushiriki kazi zao ni watunzi wa muziki, waandaaji wa muziki ikiwemo waongozaji wa video za muziki, ikiwemo waandishi wa habari za burudani na muziki.

Milango ya 'AFRIMA' ipo wazi tangu tarehe 15, Mei mwaka huu, na nafasi bado zipo kwa ushiriki hadi Julai 5 ambapo itakua mwisho wa kupokea maombi.

Utakumbuka kwamba Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizopata nafasi baada ya baadhi ya wasanii wake kutajwa kuingia katika ushiriki wa tuzo hizo, akiwemo Mrisho mpoto, Ben pol, na wengine.



Angalia mtoto alivyofanana na Haki Ngowi



Leo asubuhi Sheria Ngowi kupitia ukurasa wake wa Instagram, ameonyesha upendo kwa kutuma ujumbe kwa Haki Ngowi Ambaye ni kaka yake, akimpongeza kw malezi ya mwanae wa kiume ambae leo ni siku yake ya kuzaliwa.

Michaellukindo.blogspot.com inaungana na Sheria Ngowi kumpongeza Rian, katika siku yake ya kuzaliwa yani leo. Happy Birthday Rian, na hongera Haki Ngowi.

Alhamisi, 10 Julai 2014

Selena Gomez bado anamzimia Bieber

Kuna mambo mengi ambayo Justin Biber amekuwa akiyafanya na yakamfanya awe kwenye headlines za vyombo mbalimbali vya habari.

Utakumbuka kuna wakati Bieber alishtakiwa kwa kutupa mayai kwenye nyumba ya jirani yake hadi akapewa adhabu ya kifungo cha nje.

Wakati wote huu imeonekana kwamba mahusiano ya Bieber na Selena Gomez yanasua sua.

Kama umewahi kufuatilia kwa ufupi Justin Bieber na Selena Gomez wamewahi kuwa wapenzi na kuna wakati waliwahi kupeana makavu kila mtu akashika hamsini zake.

Chanzo cha ugomvi wao ilitokana na uhuni wa Bieber, mara zote alifanya tofauti na walivyo kubaliana.

Selena Gomez bado anamzimia Bieber na huenda mahusiano yao wanajua wenyewe namna wanavyo yaendesha. Mashabiki wao wametoa maoni kuonyesha hisia zao na inaonekana kwamba wengi hawamsapoti Selena Gomez kuendelea kuhangaika na Bieber.


Jumamosi, 5 Julai 2014

Picha: Neymar amaliza vibaya


Kwenye Picha, mchezaji wa Brazil Neymar akiwa amedondoka baada ya kuhisi maumivu kwenye uti wa mgongo

Mashabiki wa timu ya Brazil wakiwa nje ya  hospitali ya Sao Carlos 

Ijumaa, 4 Julai 2014

Video: Ed Sheeran - Drunk (Cover by Hisia)

Pg ya Twitter ya Sony Music Africa imekuwa verified leo!


Angalia Jason Derulo akiwafundisha watangazaji wa Good morning America kucheza #Wiggle




Ahadi ya Zitto Kabwe kutolea ufafanuzi ishu ya Statoil


Audio: Shaa - Subira


Kuhusu fununu za msanii wa Uganda, Cindy kushikiliwa DRS Congo

Kufuatia fununu zilizoenea kuhusu kutekwa kwa Star wa Rnb nchini Uganda Cindy, msemaje wake amezungumza.

Ufafanuzi unabainisha kwamba Cindy alipata mkataba wa kwenda kupiga show nchini Congo  ambayo ingefanyika June 30, siku ya Jumatatu.

Baada ya Cindy na Team yake kufika Congo DRC, promoter aliendaa concert akaibua jipya kwa kudai kwamba amesogeza show hadi July  5, ishu ambayo ilizua mvutano kutokana na Cindy kudai kuwa yupo booked kwenye show nyingine.

Kutoafikiana kukamfanya promoter huyo mkongo kushikilia passport ya Cindy pamoja na maneja wake, na ndio Cindy akafikia kufanya mawasiliano na ubalozi wa Uganda uliopo Kinshasa ambao nao waliwasiliana na Gavana wa Lubumbashi ambae ndio alikuja kuwanusuru.

Maandalizi ya safari yalifanyika mara moja na taarifa kutoka kwa msemaji wake zinafafanua kwamba Cindy jana usiku aliwasili Kigali, Rwanda kuungana na wasanii wengine kama Davido, ambapo wata tumbuiza kwenye sherehe za 20 za ukombozi wa Rwanda zitakazo fanyika Amahooro stadium.

Alhamisi, 3 Julai 2014

Magaidi watishia kufanya shambulio uwanja wa ndege Entebe Uganda

Ubalozi wa Marekani Uganda umetoa tahadhari kwa raia wa Uganda kuhusu tishio lililotolewa na kundi linadhaniwa kuwa ni la kigaidi, kulipua uwanja wa ndege leo usiku.