Mtangazaji maarufu wa kituo cha Televisheni cha ITV Jijini
Dar es salaam Tanzania Bw. Rainfred Masako, hivi karibuni ametoa mpya ya mwaka
kwa kumfungukia mwandishi wa michaellukindo.blogspot.com kwamba mtu kuwa na
gari ni ufahari.
Masako ambae makazi yake ni maeneo ya Mbagala, amekuwa
akimaliza soli ya kiatu kwa miaka mingi licha ya umaarufu na uzoefu wake mkubwa
utokanao na staili yake ya utangazaji, alidai kuwa alishawahi kumiliki gari
lakini hakuona tena haja ya kuendelea kuwa na gari hilo baada ya kupata
usumbufu mkubwa.
Akizungumza kwa njia ya simu Masako alisema, “Niliwahi kupata mkopo wa SACCOS ofisini
kwetu nikanunua gari kwa mtu ilikuwa mwaka 1997, lakini baadae ile gari ikaanza
kunisumbua kwa hitilafu za mara kwa mara za kiufundi kwahiyo mwaka 2001 ikabidi
niuze”, Alisema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni