Mtunzi bora wa Mwaka wa Bendi, Raisi wa Malaika Bendi Christian
Bella, amesema aliandika mashairi ya wimbo wake mpya uliotoka hivi karibuni
uitwao ‘Nani kama Mama’, kuelezea hisia
zake za dhati juu ya umuhimu wa kuheshimu na kuthamini Mama zetu, baada ya kushudia tabu aliyoipata
mke wake wakati akijifungua Mtoto Hospitalini.
Christian Bella ambae amewahi kupata tuzo ya heshima kutoka
kampuni ya First Entertainment inayofanya kazi zake chini ya Mkurugenzi Pauline
Daniel, aliyasema hayo siku chache baada ya kujaaliwa kupata Mtoto wa Pili na
mkewe (Jina tunalo).
“Nilipata nafasi kuwepo
wakati mke wangu akijifungua Mtoto Leba, nikawa nashuhudia kila kitu
kinachoendelea, yani jicho lilinitoka siwezi kusahau nilikaa pembeni
nikaangalia kwa uchungu, iliniuma sana na hapo nikazidi kupata nini maana ya
thamani ya Mama”, Alisema Christian Bella.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni