Miezi miwili iliyopita baada ya Star wa filamu za kibongo aliyewahi
kutamba na kundi la Kaole la Jijini Dar, Halima Yahaya ‘Davina’ kufunga ndoa
kimyakimya, fununu zimeibuka kwamba muigizaji huyo hakumwalika harusini swahiba
wake Salama Salmini ‘Sandra’ licha ya kwamba ndie aliye muonganishia kwa bwana
harusi.
Taarifa hizi zinaonyesha kuwepo kwa dalili za uhalisia wa tukio hilo
kutokana na tetesi kwamba wawili hao (Davina na Sandra) walijaribu kila mmoja
kwa wakati wake kumshawishi mwanaume huyo ambae jina lake halikuwekwa wazi na
mwishowe bahati kuangukia kwa Davina
Kabla ya fununu za mchapo huu kuibuka Davina aliwahi kukaririwa akisema,
“Siku moja tulitoka
na mchumba wangu (sasa mumewe) pamoja na Sandra ili kupata chakula cha jioni,
Sandra akawa anataka kuongea pembeni na mchumba wangu jambo ambalo sikulipenda
hata chembe, nikamkataza ndiyo akakasirika,”.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni