Idadi ya Likizo za Lady Jay Dee kwenda nchi za nje kila
mwaka zimemfanya Gadner G. Habash ambae ni mume wake wa ndoa kuchukua hatua ya kupaza sauti na kuvunja ukimya akidai kupatwa na wivu wa mapenzi na hali
inayoashiria upweke, hasa Jay Dee anaposafiri peke yake.
Gadner
anafunguka kwamba Lady Jay Dee husafiri kila mwaka ndani ya nyakati tofauti na
kuspendi muda wake kwa wiki kadhaa akiwa huko nje ya nchi, na kwamba kwake hazitafsiriwi
kama safari bali likizo ambazo hujitokeza katika nyakati za ‘Off Season’.
Baada
ya kudadisi ili kufahamu kwanini Lady Jay Dee huchagua mwezi wa Ramadhani kila
mwaka kusafiri nje ya nchi kwa mapumziko, Gadner alisema,
“Yeye mwenyewe kwa kuheshimu mwezi mtukufu wa Ramadhani
ambao anaona wateja wake wengine wanakua wamefunga huwa anaona anyamaze tu
kuliko kupigizana nao makelele anaona kama ni kitu ambacho sio hekima kutoa
maburudani kwa wakati huo”.
Katika
mazungumzo hayo Gadner anaendelea kusema, “Jay Dee huenda Likizo hata nyakati
nyingine mfano mwezi Januari ambao ni ‘OFF SEASON’, si kipindi cha msimu saaana
wa maburudani na hata Ramadhani ikifika japokuwa hafanyi kazi akaamua akae tu
nyumbani kwahiyo ni kwasababu ndio msimu ambao unapungua sana kutokana na aina
ya biashara anayoifanya”.
Akitoa
mifano Gadner alisema kuwa aliwahi kuongozana na mkewe Jay Dee, (Cape Town)
Africa Kusini, ikiwemo kutembelea hifadhi ya Mlima Kilimanjaro, na kudai kuwa mke
wake wakati mwingine husafiri hata kwenda China, na Ufaransa, ingawa hupendelea
Marekani zaidi kwasababu huko ana ndugu wengi wa familia yao.
Aidha
Gadner anakiri kutokuwa na tatizo dhidi ya watu wanaozungumzia sehemu ya maisha
binafsi ya ndoa yao hususani vijembe kuhusu kutokuwa na familia (watoto) na Jay
Dee, akifafanua kwamba unapokuwa kwenye ‘Spotlight’ si rahisi kuepuka kukutana
na hali hiyo.
“Mimi sina
tatizo kwa kweli kama mtu akizungumza; kibinadamu tumeumbwa hivyo ujue wakati
mwingine vinakuja positive wakati mwingine negative basi unakaza roho tu na
kuendelea na kazi, havikwepeki ukishakuwa kwenye Spotlight ila tumezoea kidogo
maana ni muda mrefu tupo kwenye hii kazi ”, Alisema.
Gadner
anaeleza kwa shauku suala la mafanikio ya Lady Jay Dee, kwamba yanakuja
kutokana na msukumo wa wapenzi wa mziki wake kwa ujumla, na kudai kwamba
mafanikio yake ni mchanganyiko wa vitu vingi, ukiacha kipaji Jay Dee ana bidii
kwa hiyo vyote vinampa msukumo mzuri sana wa mafanikio.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni