Jumatano, 27 Agosti 2014

HATA SASA KAJALA KWA PETY MAN HUTII NENO


Fununu za kuwepo kwa dalili za usaliti unaofanywa na Kajala dhidi ya mumewe ambae bado anatumikia kifungo gerezani, zimejionyesha wazi siku chache baada ya Star huyo wa ‘Bongo Muvi’ kufanikiwa kumaliza tofauti yake na aliyekuwa Miss Tanzania 2006, Wema Isac Sepetu.

Hali hiyo imejitokeza katika mazingira ambayo Kajala ameonekana kurudi Endless Fame kwa mbwembwe na makonfidensi yote ikiwa ni hatua ya kumaanisha kuwa ‘yaliopita si ndwele’ hali ambayo imezaa uhusiano wa karibu kuliko kawaida baina yake na tajiri Mtoto, Petty Man.

Hata hivyo nyota huyo (Kajala) ambae amekuwa akionekana kuspendi mshiko mrefu na maraha mengi viwanja vya kijanja kufananisha na kipato anachoingiza kwenye shughuli za sanaa, alikana kabisa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Petty Man, wakati akijibu swali la ripota wetu kama wamerudi tena kushea shuka.

Petty Man ambae ni swahiba wa mmliki wa kampuni ya Endless Fame, Wema Sepetu kwenye raha na dhiki, alipovutiwa waya kujieleza nae alikiri kuwa na ‘Upendo wa Agape’ dhidi ya Kajala, akidai kwamba ukaribu wake na Star huyo wa Bongo Muvi ni wa siku nyingi na kwamba urafiki wao umekomaa kiasi ambacho anaweza kuthubutu kumweleza hata siri zake ili kupata ushauri wenye manufaa.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni