Muigizaji nyota wa filamu za kibongo Wastara Juma Issa ‘Wastara’,
hatimae ameamua kufunguka kuhusu undani wa maisha yake ya kimapenzi baada ya kuondokewa
na mume wake kipenzi Marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’, mwaka mmoja na nusu
uliopita.
Akizungumza kupitia Clouds Tv kipindi cha ‘Sporah Show’ Wastara
anaeleza kwamba katika hali ya kibinadamu haikuwa jambo rahisi kukimbilia
mahusiano mapya wakati bado alikuwa na majeraha makubwa ya kuondokewa na Mume wake
kipenzi, Sajuki.
“Nimepata
mchumba wa kiarabu na amesha nivalisha pete, ni hatua baada ya kipindi cha
mwaka mmoja na nusu kuwa peke yangu, ni wakati muafaka sasa kuendelea na maisha
mengine ya mahusiano”, Alisema Wastara.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni