Mbongofleva wa kundi la Tip Top Connection Khalid Ramadhan
Tunda maarufu ‘Tunda Man’, amesema aliacha Soka na kuchagua muziki kwasababu ya
masharti magumu wanayopewa wachezaji kama vile kutokunywa pombe na kuwa mbali
na wanawake hususani wakati wachezaji wakijiandaa kwenda ligi kambini.
Tunda Man ambae aliwahi kucheza mpira wa miguu kwenye ligi
daraja la pili 2004 kwenda 2005, chini ya kocha m’malawi, Jackson mwangama;
Aliwezeshwa na Mkuu wa shule ya Sekondari Makongo Bw. Kipingu, kuingia kwenye
timu ya Soka ya Yanga baada ya kugundua uwezo mkubwa aliokuwa nao.
“2004 Peter
Manyika ndio alikuwa anatoka anaenda uarabuni, kwa hiyo timu ilibakia na kipa
wawili tu, Mengi Matunda na Hussein Kabwe, Sasa kwasababu huwezi kucheza ligi
wakati una makipa wawili ndio hapo mimi nikachukuliwa nikapelekwa kule tukawa
makipa watatu”, Alisema Tunda Man
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni