Jumatano, 27 Agosti 2014

THEA AITOSA BONGO MUVI



Siku chache baada ya Msanii mkubwa katika anga la filamu Bongo, Ndumbangwe Misayo, ‘Thea’ kubadilishwa Jina na mumewe Michael Sangu ‘Mike’ na kuitwa Salome Urasa Sangu, muigizaji huyo juzi kati alimwagia paparazi wetu mastori kuhusu mpango ya ujio wake mpya baada ya kuwa kimya kwa kipindi kirefu.

Salome Sangu ‘Thea’ katika hali ya uchangamfu na kujiamini alikanusha mbele ya ripota wa umbea huu kuhusu fununu za kuitosa Bongo Muvi akidai kwamba kimya chake kilitokana na kugundua kuwa ni sawa na upuuzi kuonekana kila siku kwenye makava ya filamu za kibongo wakati hana pesa mfukoni.


Akiendelea kuzungumza kwa makonfidensi yote kuhusu mkakati madhubuti alioandaa dhidi ya kazi zake mpya za filamu Star huyo anasema , “Wapenzi wa Filamu za Bongo watarajie kazi nzuri kutoka kwenye kampuni yetu mimi na mume wangu,muda wowote kutoka sasa zitaanza kuingia sokoni”.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni