Mwanamitindo wa Tanzania Martin Andrew Kadinda, amewataka
watanzania kufahamu kwamba anamzimia kimapenzi Mwanamitindo maarufu, muigizaji
mkubwa wa sinema duniani Mwanamuziki nyota Marekani, anayemiliki utajiri
wa zaidi ya dola za Kimarekani 300 Milioni, Jennifer Lynn Lopez.
Akizungumza
na michaellukindo.blogspot.com Martin Kadinda (27) ambae pia ni Meneja wa aliyekuwa Miss
Tanzania 2006 Wema Isac Sepetu, alidai kwamba hajawahi kuona mwanamke mzuri
katika maisha yake kama J-Lo, na kwamba anampango wa kufanya jina lake kuwa
kubwa upesi ili aweze kukutana na Star huyo.
Mwanamitindo
huyo aliongeza msisitizo kwasema, “Mimi
naamini kila kitu ni bahati, kama nimeweza kufanya kazi na madizaina wakubwa
naamini hata hili la kutoka na Jennifer Lopez ni dogo tu kwangu”.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni