Malkia wa Mipasho nchini, Khadija Omar Kopa ‘Top in Town’ amesema
kwamba toleo jipya la Albamu yake kutakua na mabadiliko mengi ya kiufundi kama
vile kupungua kwa urefu wa nyimbo zake kutoka dakika ishirini hadi tisa kila
wimbo.
Mkali huyo alietamba na kibao cha ‘Mjini Chuo Kikuu’ amesema lengo si kupunguza raha ya
kucheza au kusikiliza muziki wa taarabu isipokuwa kuongeza hamu ya kusikiliza
nyimbo nyingi kwa muda mfupi, akifafanua kwamba wimbo unapokuwa mrefu sana
msikilizaji nae anaweza aidha kuchoka kabla wimbo haujamalizika.
“Albamu mpya ikitoka
kutakuwa na mabadiliko mengi na kubwa ni kipimo cha urefu wa nyimbo zote, watu
wataweza kusikiliza hata nyimbo tatu kwa muda mfupi. Dakika zitapungua kutoka
ishirini kwa wimbo mmoja hadi dakika tisa”, Alisema Khadija Khopa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni