Nyota wa zamani wa tamthilia ya Jumba la dhahabu, Miriam
Jolwa maarufu kama Jini kabula ameapa kutoacha kabisa tabia ya kuvaa ‘vichupi’
akionyesha msisitizo kwamba hiyo ndio aina ya maisha aliyochagua kwasababu
inamfanya awe huru.
Akistorisha na paparazi wa michaellukindo.blogspot.com msanii huyo aliendelea kusema
kwamba vichupi ndio mavazi aliyokuwa akivaa tangu enzi za Utoto wake na kwamba
hakuna mtu yoyote atakaye badili maamuzi yake kuhusu kubadili mfumo wake wa
uvaaji.
Kabula ambae hapo awali aliwahi kujiingiza kwenye sanaa ya
Muziki akiwa katika kundi la ‘Scorpion Girls’ pamoja na wasanii wengine wakike kama
Rashida Wanjara na Isabela ‘Bella’, aliweka aibu pembeni na kusema, “Binadamu wameumbwa wanasema kwahiyo waache
waseme alafu wakiona wametosheka watapiga kimyaa vichupi siachi”.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni