Ufafanuzi unabainisha kwamba Cindy alipata mkataba wa kwenda kupiga show nchini Congo ambayo ingefanyika June 30, siku ya Jumatatu.
Baada ya Cindy na Team yake kufika Congo DRC, promoter aliendaa concert akaibua jipya kwa kudai kwamba amesogeza show hadi July 5, ishu ambayo ilizua mvutano kutokana na Cindy kudai kuwa yupo booked kwenye show nyingine.
Kutoafikiana kukamfanya promoter huyo mkongo kushikilia passport ya Cindy pamoja na maneja wake, na ndio Cindy akafikia kufanya mawasiliano na ubalozi wa Uganda uliopo Kinshasa ambao nao waliwasiliana na Gavana wa Lubumbashi ambae ndio alikuja kuwanusuru.
Maandalizi ya safari yalifanyika mara moja na taarifa kutoka kwa msemaji wake zinafafanua kwamba Cindy jana usiku aliwasili Kigali, Rwanda kuungana na wasanii wengine kama Davido, ambapo wata tumbuiza kwenye sherehe za 20 za ukombozi wa Rwanda zitakazo fanyika Amahooro stadium.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni