Utakumbuka kuna wakati Bieber alishtakiwa kwa kutupa mayai kwenye nyumba ya jirani yake hadi akapewa adhabu ya kifungo cha nje.
Wakati wote huu imeonekana kwamba mahusiano ya Bieber na Selena Gomez yanasua sua.
Kama umewahi kufuatilia kwa ufupi Justin Bieber na Selena Gomez wamewahi kuwa wapenzi na kuna wakati waliwahi kupeana makavu kila mtu akashika hamsini zake.
Chanzo cha ugomvi wao ilitokana na uhuni wa Bieber, mara zote alifanya tofauti na walivyo kubaliana.
Selena Gomez bado anamzimia Bieber na huenda mahusiano yao wanajua wenyewe namna wanavyo yaendesha. Mashabiki wao wametoa maoni kuonyesha hisia zao na inaonekana kwamba wengi hawamsapoti Selena Gomez kuendelea kuhangaika na Bieber.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni