Ijumaa, 11 Julai 2014

Exclusive: AFRIMA wametangaza nafasi za ushiriki wa wazi


Tuzo za muziki 'AFRIMA' nchini marekani kwa kushirikiana na Umoja wa Africa (Africa Union) wameamua kupanua wigo wao kwa kutangaza nafasi za wazi za ushiriki wa tuzo hizo. 

Lengo kubwa ni kutoa fursa kwa wasanii mbalimbali, kukuza vipaji vya wana-sanaa wa Afrika, kuwapongeza kwa tuzo ili kuutangaza utamaduni wa nchi zao (za Afrika) ambao kirahisi utatambuliwa na dunia.

Wanaoruhusiwa kushiriki kazi zao ni watunzi wa muziki, waandaaji wa muziki ikiwemo waongozaji wa video za muziki, ikiwemo waandishi wa habari za burudani na muziki.

Milango ya 'AFRIMA' ipo wazi tangu tarehe 15, Mei mwaka huu, na nafasi bado zipo kwa ushiriki hadi Julai 5 ambapo itakua mwisho wa kupokea maombi.

Utakumbuka kwamba Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizopata nafasi baada ya baadhi ya wasanii wake kutajwa kuingia katika ushiriki wa tuzo hizo, akiwemo Mrisho mpoto, Ben pol, na wengine.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni