Jumanne, 29 Julai 2014

BABA ACHARAZA VIBOKO WALIMU

Kamanda wa Polisi Mkoani Tabora, Suzan Kaganda
Vitendo vya baadhi ya wazazi , kudhalilisha walimu vinaendelea ambapo mzazi mmoja Selemani Juma, amewashambulia walimu wawili kwa viboko.

Amefanya hivyo kupinga mwanawe kurudishwa nyumbani, akashone kaptura. Alifanya hivyo mwishoni mwa wiki iliyopita. Taarifa zinasema Juma alidhalilisha walimu wawili wa Shule ya Msingi Nzogimlole iliyopo wilayani Nzega Mkoani Tabora.

Kwa Mujibu wa Mwalimu Josephat, Mwalimu aliyeshambuliwa (Jina limehifadhiwa), alikuwa akifundisha katika darasa hilo na alipomuona mwanafunzi huyo kavaa kaptura iliyochanika vibaya, kiasi cha sehemu za siri kuonekana, alimrudisha nyumbani kwenda kurekebisha sare yake na ndipo kisanga kikamrudia.

CHANZO: GAZETI HABARI LEO. Imeandikwa na Lucas Raphael, Tabora.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni