The Official Michael Lukindo Blog
Number One for Gossip Stories | Entertainment News | Exclusive Infoz & Breaking News | Contact: +255 719 11 9210 | Email: mikewatzee@gmail.com
Jumatano, 27 Agosti 2014
VIDEO: INTERVIEW YA MIKE 100.5, TIMES FM
<iframe width="560" height="315" src="//www.youtube.com/embed/YXXvFSNJDM0" frameborder="0" allowfullscreen></iframe>
RECORDING SESSION SIKU YANGU YA KUZALIWA - JOH MAKINI
Rapa wa Kanda ya Kaskazini Joh Makini amestorisha kwamba
alianza kuwa inspired kufanya Hip hop baada ya kuwaskiliza wasanii kama Saleh
Jabir, Mr II Sugu na wengine wakinata na beat na kuamini kuwa inawezekana hata
yeye kufanya hivyo.
Mwamba anaendelea kufunguka kwa kusema kwamba ana role
models wengine wengi hata Dr dree ni moja wa Role Model wake lakini Jay z ni A
list wa Role models wake ambae bado hamfananishi na Rapaz wengine New York
Akizungumza katika siku yake ya kuzaliwa tar 27/08 kupitia
mahojiano na kipindi cha Power Jams EA Radio, Rapa huyo anasema, “Kuwa
hivi nilivyo nilijipata nafanya hivi, ni kitu ambacho hakielezeki”.
Aidha Mwamba amekazia kwamba leo itakuwa mara ya kwanza kufanya Studio Session na Producer Marco Chali katika rekodi ya siku yake ya kuzaliwa jambo ambalo litabaki kuwa kumbukumbu.
Visit: www.michaellukindo.com
DAVINA: SANDRA ALIDHANI SITAOLEWA
Miezi miwili iliyopita baada ya Star wa filamu za kibongo aliyewahi
kutamba na kundi la Kaole la Jijini Dar, Halima Yahaya ‘Davina’ kufunga ndoa
kimyakimya, fununu zimeibuka kwamba muigizaji huyo hakumwalika harusini swahiba
wake Salama Salmini ‘Sandra’ licha ya kwamba ndie aliye muonganishia kwa bwana
harusi.
Taarifa hizi zinaonyesha kuwepo kwa dalili za uhalisia wa tukio hilo
kutokana na tetesi kwamba wawili hao (Davina na Sandra) walijaribu kila mmoja
kwa wakati wake kumshawishi mwanaume huyo ambae jina lake halikuwekwa wazi na
mwishowe bahati kuangukia kwa Davina
Kabla ya fununu za mchapo huu kuibuka Davina aliwahi kukaririwa akisema,
“Siku moja tulitoka
na mchumba wangu (sasa mumewe) pamoja na Sandra ili kupata chakula cha jioni,
Sandra akawa anataka kuongea pembeni na mchumba wangu jambo ambalo sikulipenda
hata chembe, nikamkataza ndiyo akakasirika,”.
HATA SASA KAJALA KWA PETY MAN HUTII NENO
Fununu za kuwepo kwa dalili za usaliti unaofanywa na Kajala
dhidi ya mumewe ambae bado anatumikia kifungo gerezani, zimejionyesha wazi
siku chache baada ya Star huyo wa ‘Bongo Muvi’ kufanikiwa kumaliza tofauti yake
na aliyekuwa Miss Tanzania 2006, Wema Isac Sepetu.
Hali hiyo imejitokeza katika mazingira ambayo Kajala
ameonekana kurudi Endless Fame kwa mbwembwe na makonfidensi yote ikiwa ni hatua
ya kumaanisha kuwa ‘yaliopita si ndwele’ hali ambayo imezaa uhusiano wa karibu
kuliko kawaida baina yake na tajiri Mtoto, Petty Man.
Hata hivyo nyota huyo (Kajala) ambae amekuwa akionekana
kuspendi mshiko mrefu na maraha mengi viwanja vya kijanja kufananisha na kipato
anachoingiza kwenye shughuli za sanaa, alikana kabisa kuwa na mahusiano ya
kimapenzi na Petty Man, wakati akijibu swali la ripota wetu kama wamerudi tena
kushea shuka.
Petty Man ambae ni swahiba wa mmliki wa kampuni ya Endless
Fame, Wema Sepetu kwenye raha na dhiki, alipovutiwa waya kujieleza nae alikiri
kuwa na ‘Upendo wa Agape’ dhidi ya Kajala, akidai kwamba ukaribu wake
na Star huyo wa Bongo Muvi ni wa siku nyingi na kwamba urafiki wao umekomaa
kiasi ambacho anaweza kuthubutu kumweleza hata siri zake ili kupata ushauri
wenye manufaa.
JINI KABULA AJISIFIA KUVAA NUSU UTUPU
Nyota wa zamani wa tamthilia ya Jumba la dhahabu, Miriam
Jolwa maarufu kama Jini kabula ameapa kutoacha kabisa tabia ya kuvaa ‘vichupi’
akionyesha msisitizo kwamba hiyo ndio aina ya maisha aliyochagua kwasababu
inamfanya awe huru.
Akistorisha na paparazi wa michaellukindo.blogspot.com msanii huyo aliendelea kusema
kwamba vichupi ndio mavazi aliyokuwa akivaa tangu enzi za Utoto wake na kwamba
hakuna mtu yoyote atakaye badili maamuzi yake kuhusu kubadili mfumo wake wa
uvaaji.
Kabula ambae hapo awali aliwahi kujiingiza kwenye sanaa ya
Muziki akiwa katika kundi la ‘Scorpion Girls’ pamoja na wasanii wengine wakike kama
Rashida Wanjara na Isabela ‘Bella’, aliweka aibu pembeni na kusema, “Binadamu wameumbwa wanasema kwahiyo waache
waseme alafu wakiona wametosheka watapiga kimyaa vichupi siachi”.
MKE WA MTU MTAMU - TIMBULO
Wakati vyombo vya habari vikikemea tabia zinazochochea
vitendo vya ngono nje ya ndoa ili kuepuka UKIMWI, msanii wa kizazi kipya
maarufu Timbulo, ameonyesha udhaifu wake kwa kiasi kikubwa kueleza namna
ambavyo amekua akichepuka na mke wa mtu.
Timbulo alikiri kufanya vitendo hivyo vichafu na mke wa mtu
akidai kuwa aliweza kulala na kishtobe huyo wakati wowote alipojiskia na kwamba
hakuwahi kuwa na hofu juu suala la fumanizi.
“Ni kweli nilikuwa natoka na mwanadada ambaye ni mke wa mtu, ila nilikuwa
sifahamu chochote kwasababu muda wowote nikimuhitaji nilimpata”,Alisema
Msanii huyo anajisahau zaidi na kumueleza ripota wa
michaellukindo.blogspot.com kwamba ilifika wakati mwenye mke aligundua na kumuonya juu
ya tabia yake ya uzinzi, hatua iliyompa woga hadi kufikia kuacha vitendo hivyo
vya ngono zembe.
THEA AITOSA BONGO MUVI
Siku chache baada ya Msanii mkubwa katika anga la filamu
Bongo, Ndumbangwe Misayo, ‘Thea’ kubadilishwa Jina na mumewe Michael Sangu
‘Mike’ na kuitwa Salome Urasa Sangu, muigizaji huyo juzi kati alimwagia
paparazi wetu mastori kuhusu mpango ya ujio wake mpya baada ya kuwa kimya kwa
kipindi kirefu.
Salome Sangu ‘Thea’ katika hali ya uchangamfu na kujiamini alikanusha
mbele ya ripota wa umbea huu kuhusu fununu za kuitosa Bongo Muvi akidai kwamba
kimya chake kilitokana na kugundua kuwa ni sawa na upuuzi kuonekana kila siku
kwenye makava ya filamu za kibongo wakati hana pesa mfukoni.
Akiendelea kuzungumza kwa makonfidensi yote kuhusu mkakati
madhubuti alioandaa dhidi ya kazi zake mpya za filamu Star huyo anasema , “Wapenzi wa Filamu za Bongo watarajie kazi
nzuri kutoka kwenye kampuni yetu mimi na mume wangu,muda wowote kutoka sasa
zitaanza kuingia sokoni”.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)