Jumatano, 27 Agosti 2014

VIDEO: INTERVIEW YA MIKE 100.5, TIMES FM

<iframe width="560" height="315" src="//www.youtube.com/embed/YXXvFSNJDM0" frameborder="0" allowfullscreen></iframe>

RECORDING SESSION SIKU YANGU YA KUZALIWA - JOH MAKINI


Rapa wa Kanda ya Kaskazini Joh Makini amestorisha kwamba alianza kuwa inspired kufanya Hip hop baada ya kuwaskiliza wasanii kama Saleh Jabir, Mr II Sugu na wengine wakinata na beat na kuamini kuwa inawezekana hata yeye kufanya hivyo.

Mwamba anaendelea kufunguka kwa kusema kwamba ana role models wengine wengi hata Dr dree ni moja wa Role Model wake lakini Jay z ni A list wa Role models wake ambae bado hamfananishi na Rapaz wengine New York

Akizungumza katika siku yake ya kuzaliwa tar 27/08 kupitia mahojiano na kipindi cha Power Jams EA Radio, Rapa huyo anasema, “Kuwa hivi nilivyo nilijipata nafanya hivi, ni kitu ambacho hakielezeki”.

Aidha Mwamba amekazia kwamba leo itakuwa mara ya kwanza kufanya Studio Session na Producer Marco Chali katika rekodi ya siku yake ya kuzaliwa jambo ambalo litabaki kuwa kumbukumbu.

Visit: www.michaellukindo.com

DAVINA: SANDRA ALIDHANI SITAOLEWA


Miezi miwili iliyopita baada ya Star wa filamu za kibongo aliyewahi kutamba na kundi la Kaole la Jijini Dar, Halima Yahaya ‘Davina’ kufunga ndoa kimyakimya, fununu zimeibuka kwamba muigizaji huyo hakumwalika harusini swahiba wake Salama Salmini ‘Sandra’ licha ya kwamba ndie aliye muonganishia kwa bwana harusi.
Taarifa hizi zinaonyesha kuwepo kwa dalili za uhalisia wa tukio hilo kutokana na tetesi kwamba wawili hao (Davina na Sandra) walijaribu kila mmoja kwa wakati wake kumshawishi mwanaume huyo ambae jina lake halikuwekwa wazi na mwishowe bahati kuangukia kwa Davina
Kabla ya fununu za mchapo huu kuibuka Davina aliwahi kukaririwa akisema, Siku moja tulitoka na mchumba wangu (sasa mumewe) pamoja na Sandra ili kupata chakula cha jioni, Sandra akawa anataka kuongea pembeni na mchumba wangu jambo ambalo sikulipenda hata chembe, nikamkataza ndiyo akakasirika,”.


HATA SASA KAJALA KWA PETY MAN HUTII NENO


Fununu za kuwepo kwa dalili za usaliti unaofanywa na Kajala dhidi ya mumewe ambae bado anatumikia kifungo gerezani, zimejionyesha wazi siku chache baada ya Star huyo wa ‘Bongo Muvi’ kufanikiwa kumaliza tofauti yake na aliyekuwa Miss Tanzania 2006, Wema Isac Sepetu.

Hali hiyo imejitokeza katika mazingira ambayo Kajala ameonekana kurudi Endless Fame kwa mbwembwe na makonfidensi yote ikiwa ni hatua ya kumaanisha kuwa ‘yaliopita si ndwele’ hali ambayo imezaa uhusiano wa karibu kuliko kawaida baina yake na tajiri Mtoto, Petty Man.

Hata hivyo nyota huyo (Kajala) ambae amekuwa akionekana kuspendi mshiko mrefu na maraha mengi viwanja vya kijanja kufananisha na kipato anachoingiza kwenye shughuli za sanaa, alikana kabisa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Petty Man, wakati akijibu swali la ripota wetu kama wamerudi tena kushea shuka.

Petty Man ambae ni swahiba wa mmliki wa kampuni ya Endless Fame, Wema Sepetu kwenye raha na dhiki, alipovutiwa waya kujieleza nae alikiri kuwa na ‘Upendo wa Agape’ dhidi ya Kajala, akidai kwamba ukaribu wake na Star huyo wa Bongo Muvi ni wa siku nyingi na kwamba urafiki wao umekomaa kiasi ambacho anaweza kuthubutu kumweleza hata siri zake ili kupata ushauri wenye manufaa.


JINI KABULA AJISIFIA KUVAA NUSU UTUPU


Nyota wa zamani wa tamthilia ya Jumba la dhahabu, Miriam Jolwa maarufu kama Jini kabula ameapa kutoacha kabisa tabia ya kuvaa ‘vichupi’ akionyesha msisitizo kwamba hiyo ndio aina ya maisha aliyochagua kwasababu inamfanya awe huru.

Akistorisha na paparazi wa michaellukindo.blogspot.com msanii huyo aliendelea kusema kwamba vichupi ndio mavazi aliyokuwa akivaa tangu enzi za Utoto wake na kwamba hakuna mtu yoyote atakaye badili maamuzi yake kuhusu kubadili mfumo wake wa uvaaji.

Kabula ambae hapo awali aliwahi kujiingiza kwenye sanaa ya Muziki akiwa katika kundi la ‘Scorpion Girls’ pamoja na wasanii wengine wakike kama Rashida Wanjara na Isabela ‘Bella’, aliweka aibu pembeni na kusema, “Binadamu wameumbwa wanasema kwahiyo waache waseme alafu wakiona wametosheka watapiga kimyaa vichupi siachi”.



MKE WA MTU MTAMU - TIMBULO


Wakati vyombo vya habari vikikemea tabia zinazochochea vitendo vya ngono nje ya ndoa ili kuepuka UKIMWI, msanii wa kizazi kipya maarufu Timbulo, ameonyesha udhaifu wake kwa kiasi kikubwa kueleza namna ambavyo amekua akichepuka na mke wa mtu.

Timbulo alikiri kufanya vitendo hivyo vichafu na mke wa mtu akidai kuwa aliweza kulala na kishtobe huyo wakati wowote alipojiskia na kwamba hakuwahi kuwa na hofu juu suala la fumanizi.

“Ni kweli nilikuwa natoka na mwanadada ambaye ni mke wa mtu, ila nilikuwa sifahamu chochote kwasababu muda wowote nikimuhitaji nilimpata”,Alisema

Msanii huyo anajisahau zaidi na kumueleza ripota wa michaellukindo.blogspot.com kwamba ilifika wakati mwenye mke aligundua na kumuonya juu ya tabia yake ya uzinzi, hatua iliyompa woga hadi kufikia kuacha vitendo hivyo vya ngono zembe.


THEA AITOSA BONGO MUVI



Siku chache baada ya Msanii mkubwa katika anga la filamu Bongo, Ndumbangwe Misayo, ‘Thea’ kubadilishwa Jina na mumewe Michael Sangu ‘Mike’ na kuitwa Salome Urasa Sangu, muigizaji huyo juzi kati alimwagia paparazi wetu mastori kuhusu mpango ya ujio wake mpya baada ya kuwa kimya kwa kipindi kirefu.

Salome Sangu ‘Thea’ katika hali ya uchangamfu na kujiamini alikanusha mbele ya ripota wa umbea huu kuhusu fununu za kuitosa Bongo Muvi akidai kwamba kimya chake kilitokana na kugundua kuwa ni sawa na upuuzi kuonekana kila siku kwenye makava ya filamu za kibongo wakati hana pesa mfukoni.


Akiendelea kuzungumza kwa makonfidensi yote kuhusu mkakati madhubuti alioandaa dhidi ya kazi zake mpya za filamu Star huyo anasema , “Wapenzi wa Filamu za Bongo watarajie kazi nzuri kutoka kwenye kampuni yetu mimi na mume wangu,muda wowote kutoka sasa zitaanza kuingia sokoni”.

RAINFRED MASAKO ADAI KUWA NA GARI NI UFAHARI


Mtangazaji maarufu wa kituo cha Televisheni cha ITV Jijini Dar es salaam Tanzania Bw. Rainfred Masako, hivi karibuni ametoa mpya ya mwaka kwa kumfungukia mwandishi wa michaellukindo.blogspot.com kwamba mtu kuwa na gari ni ufahari.

Masako ambae makazi yake ni maeneo ya Mbagala, amekuwa akimaliza soli ya kiatu kwa miaka mingi licha ya umaarufu na uzoefu wake mkubwa utokanao na staili yake ya utangazaji, alidai kuwa alishawahi kumiliki gari lakini hakuona tena haja ya kuendelea kuwa na gari hilo baada ya kupata usumbufu mkubwa.

Akizungumza kwa njia ya simu Masako alisema, “Niliwahi kupata mkopo wa SACCOS ofisini kwetu nikanunua gari kwa mtu ilikuwa mwaka 1997, lakini baadae ile gari ikaanza kunisumbua kwa hitilafu za mara kwa mara za kiufundi kwahiyo mwaka 2001 ikabidi niuze”, Alisema.


CHRISTIAN BELLA AZAMIA LEBA, JICHO LAMTOKA KAMA NGUMI


Mtunzi bora wa Mwaka wa Bendi, Raisi wa Malaika Bendi Christian Bella, amesema aliandika mashairi ya wimbo wake mpya uliotoka hivi karibuni uitwao ‘Nani kama Mama’,  kuelezea hisia zake za dhati juu ya umuhimu wa kuheshimu na kuthamini  Mama zetu, baada ya kushudia tabu aliyoipata mke wake wakati akijifungua Mtoto Hospitalini.

Christian Bella ambae amewahi kupata tuzo ya heshima kutoka kampuni ya First Entertainment inayofanya kazi zake chini ya Mkurugenzi Pauline Daniel, aliyasema hayo siku chache baada ya kujaaliwa kupata Mtoto wa Pili na mkewe (Jina tunalo).


Nilipata nafasi kuwepo wakati mke wangu akijifungua Mtoto Leba, nikawa nashuhudia kila kitu kinachoendelea, yani jicho lilinitoka siwezi kusahau nilikaa pembeni nikaangalia kwa uchungu, iliniuma sana na hapo nikazidi kupata nini maana ya thamani ya Mama”, Alisema Christian Bella.

Jumatatu, 25 Agosti 2014

FUPI TAMU JAMANI NDEFU INABOA - KHADIJA KOPA


Malkia wa Mipasho nchini, Khadija Omar Kopa ‘Top in Town’ amesema kwamba toleo jipya la Albamu yake kutakua na mabadiliko mengi ya kiufundi kama vile kupungua kwa urefu wa nyimbo zake kutoka dakika ishirini hadi tisa kila wimbo.

Mkali huyo alietamba na kibao cha Mjini Chuo Kikuu amesema lengo si kupunguza raha ya kucheza au kusikiliza muziki wa taarabu isipokuwa kuongeza hamu ya kusikiliza nyimbo nyingi kwa muda mfupi, akifafanua kwamba wimbo unapokuwa mrefu sana msikilizaji nae anaweza aidha kuchoka kabla wimbo haujamalizika.

Albamu mpya ikitoka kutakuwa na mabadiliko mengi na kubwa ni kipimo cha urefu wa nyimbo zote, watu wataweza kusikiliza hata nyimbo tatu kwa muda mfupi. Dakika zitapungua kutoka ishirini kwa wimbo mmoja hadi dakika tisa”, Alisema Khadija Khopa.



ONA JINSI LADY JAY DEE ANAVYOMTESA GADNA WAKE


Idadi ya Likizo za Lady Jay Dee kwenda nchi za nje kila mwaka zimemfanya Gadner G. Habash ambae ni mume wake wa ndoa kuchukua hatua ya kupaza sauti na kuvunja ukimya akidai kupatwa na wivu wa mapenzi na hali inayoashiria upweke, hasa Jay Dee anaposafiri peke yake.

Gadner anafunguka kwamba Lady Jay Dee husafiri kila mwaka ndani ya nyakati tofauti na kuspendi muda wake kwa wiki kadhaa akiwa huko nje ya nchi, na kwamba kwake hazitafsiriwi kama safari bali likizo ambazo hujitokeza katika nyakati za ‘Off Season’.

Baada ya kudadisi ili kufahamu kwanini Lady Jay Dee huchagua mwezi wa Ramadhani kila mwaka kusafiri nje ya nchi kwa mapumziko, Gadner alisema,

Yeye mwenyewe kwa kuheshimu mwezi mtukufu wa Ramadhani ambao anaona wateja wake wengine wanakua wamefunga huwa anaona anyamaze tu kuliko kupigizana nao makelele anaona kama ni kitu ambacho sio hekima kutoa maburudani kwa wakati huo.

Katika mazungumzo hayo Gadner anaendelea kusema, Jay Dee huenda Likizo hata nyakati nyingine mfano mwezi Januari ambao ni ‘OFF SEASON’, si kipindi cha msimu saaana wa maburudani na hata Ramadhani ikifika japokuwa hafanyi kazi akaamua akae tu nyumbani kwahiyo ni kwasababu ndio msimu ambao unapungua sana kutokana na aina ya biashara anayoifanya”.

Akitoa mifano Gadner alisema kuwa aliwahi kuongozana na mkewe Jay Dee, (Cape Town) Africa Kusini, ikiwemo kutembelea hifadhi ya Mlima Kilimanjaro, na kudai kuwa mke wake wakati mwingine husafiri hata kwenda China, na Ufaransa, ingawa hupendelea Marekani zaidi kwasababu huko ana ndugu wengi wa familia yao.

Aidha Gadner anakiri kutokuwa na tatizo dhidi ya watu wanaozungumzia sehemu ya maisha binafsi ya ndoa yao hususani vijembe kuhusu kutokuwa na familia (watoto) na Jay Dee, akifafanua kwamba unapokuwa kwenye ‘Spotlight’ si rahisi kuepuka kukutana na hali hiyo.

Mimi sina tatizo kwa kweli kama mtu akizungumza; kibinadamu tumeumbwa hivyo ujue wakati mwingine vinakuja positive wakati mwingine negative basi unakaza roho tu na kuendelea na kazi, havikwepeki ukishakuwa kwenye Spotlight ila tumezoea kidogo maana ni muda mrefu tupo kwenye hii kazi ”, Alisema.


Gadner anaeleza kwa shauku suala la mafanikio ya Lady Jay Dee, kwamba yanakuja kutokana na msukumo wa wapenzi wa mziki wake kwa ujumla, na kudai kwamba mafanikio yake ni mchanganyiko wa vitu vingi, ukiacha kipaji Jay Dee ana bidii kwa hiyo vyote vinampa msukumo mzuri sana wa mafanikio.

ULE UCHUMBA NA PETE ALIYOVISHWA WASTARA!!!



Muigizaji nyota wa filamu za kibongo Wastara Juma Issa ‘Wastara’, hatimae ameamua kufunguka kuhusu undani wa maisha yake ya kimapenzi baada ya kuondokewa na mume wake kipenzi Marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’, mwaka mmoja na nusu uliopita.

Akizungumza kupitia Clouds Tv kipindi cha ‘Sporah Show’ Wastara anaeleza kwamba katika hali ya kibinadamu haikuwa jambo rahisi kukimbilia mahusiano mapya wakati bado alikuwa na majeraha makubwa ya kuondokewa na Mume wake kipenzi, Sajuki.


“Nimepata mchumba wa kiarabu na amesha nivalisha pete, ni hatua baada ya kipindi cha mwaka mmoja na nusu kuwa peke yangu, ni wakati muafaka sasa kuendelea na maisha mengine ya mahusiano”, Alisema Wastara.

EXCLUSIVE: KUMBE BINTI KIZIWI ALIZAA NA MUHOLANZI, SOMA ZAIDI UFAHAMU MENGI


ALIKUA AKIJIUZA VISIWANI ZANZIBAR, ALIZAA NA MUHOLANZI

·         Alimuhonga mihela kibao ili aache umalaya lakini wapi
·         Mzungu ajuta kumjua/astaajabu licha ya ujauzito bado binti atinga viwanja usiku wa manane na tumbo lake
·         Tamaa zamponza kama fisi mzungu am'bwaga akacha


Hatimae siri imefichuka kuhusu historia ya maisha ya Sabra Khan maarufu ‘binti kiziwi’msichana aliyewahi kujipatia umaarufu mkubwa mara baada ya kushirikishwa kama Video Qeen kwenye nyimbo ya msanii wa kizazi kipya Z-Anto

Chaumbea mmoja aliebobea alivujisha kwa raha zake siri za binti kiziwi akidai kwamba kabla ya shostito huyo kujizolea umaarufu mkubwa nchini kwa kusafiria nyota ya Z-Anto, aliwahi kuishi Visiwani Zanzibar ambako inasemekana alikuwa akijihusisha na shughuli za ukahaba.

Mpashaji huyo alikamia kusimulia akikazia kuwa katika harakati za Binti kiziwi kujirusha sana viwanja vya starehe akiuza uroda, alianza kuwa bwege wa ngono zembe na mwishoe kugeuka teja wa ngono kwenye ngozi ya mteja anaedaiwa kuwa ni mzungu, raia wa Uholanzi ambapo mwishoe alinasa ki zaigoti aka ujauzito

"Mtoto wa kike kiguu na njia tumbo limekua kubwa, mzungu anahudumia kwa mbwembwe na kiingereza chote lakini mwanamke kama zoba vile yani usiku anatoroka unamkuta viwanja anakula vichwa", Alisema mpashaji huyo.

Kama ambavyo waswahili husema 'kunguru hafugiki' unaambiwa mtoto alipozaliwa baada ya mtasha kuona kicheche hasomeki aliamua bora amchukue mwanae na kutokomoea nae kimya kimya nyumbani kwao uholanzi.

Endapo utakua ni mfuatiliaji mzuri mapema mwaka huu mlimbwende Sabra Khan aka Binti kiziwi aliandikwa na kutajwa mara nyingi sana kwenye vyombo vya habari akihusishwa na tuhuma za kunaswa na dawa za kulevya huko China.

Wajuzi wa mambo wanaeleza kwamba huenda shostito huyo mwenye uraia wa Tanzania akawa alinyongwa kutokana na sheria za Jamuhuri ya china hasa unaponyakwa ukijihusisha na biashara haramu.

Rafiki wa karibu kabisa na binti kiziwi ambaye yupo hapa nchini alimfungukia mwandishi wetu akimlaani bibie Jackline Patrick aka sikio la kufa akidai kuwa yeye ndiye alimbebesha binti kiziwi mzigo huo wa madawa na kumtelekeza baada ya kubainika na kutiwa kwenye nguvu ya dola.


Jumapili, 24 Agosti 2014

POMBE, WANAWAKE VYAMPONZA TUNDA MAN KUACHA SOKA


Mbongofleva wa kundi la Tip Top Connection Khalid Ramadhan Tunda maarufu ‘Tunda Man’, amesema aliacha Soka na kuchagua muziki kwasababu ya masharti magumu wanayopewa wachezaji kama vile kutokunywa pombe na kuwa mbali na wanawake hususani wakati wachezaji wakijiandaa kwenda ligi kambini.

Tunda Man ambae aliwahi kucheza mpira wa miguu kwenye ligi daraja la pili 2004 kwenda 2005, chini ya kocha m’malawi, Jackson mwangama; Aliwezeshwa na Mkuu wa shule ya Sekondari Makongo Bw. Kipingu, kuingia kwenye timu ya Soka ya Yanga baada ya kugundua uwezo mkubwa aliokuwa nao.


“2004 Peter Manyika ndio alikuwa anatoka anaenda uarabuni, kwa hiyo timu ilibakia na kipa wawili tu, Mengi Matunda na Hussein Kabwe, Sasa kwasababu huwezi kucheza ligi wakati una makipa wawili ndio hapo mimi nikachukuliwa nikapelekwa kule tukawa makipa watatu”, Alisema Tunda Man

PENZI LA JENNIFER LOPEZ LAMTESA MWANAMITINDO MARTIN KADINDA


Mwanamitindo wa Tanzania Martin Andrew Kadinda, amewataka watanzania kufahamu kwamba anamzimia kimapenzi Mwanamitindo maarufu, muigizaji mkubwa wa sinema duniani Mwanamuziki nyota Marekani, anayemiliki utajiri wa zaidi ya dola za Kimarekani 300 Milioni, Jennifer Lynn Lopez.

Akizungumza na michaellukindo.blogspot.com Martin Kadinda (27) ambae pia ni Meneja wa aliyekuwa Miss Tanzania 2006 Wema Isac Sepetu, alidai kwamba hajawahi kuona mwanamke mzuri katika maisha yake kama J-Lo, na kwamba anampango wa kufanya jina lake kuwa kubwa upesi ili aweze kukutana na Star huyo.


Mwanamitindo huyo aliongeza msisitizo kwasema, “Mimi naamini kila kitu ni bahati, kama nimeweza kufanya kazi na madizaina wakubwa naamini hata hili la kutoka na Jennifer Lopez ni dogo tu kwangu”.

Jumanne, 19 Agosti 2014

KESI MPYA INAYOMKABILI R. KELLY



R. Kelly anatajwa kuwa mtu asie na shukrani kwa mtu aliemtoa na kumfanya awe Star ni taarifa iliyoibuka kutoakana na kesi mpya inayomkabili super nyota huyo.

Derrel McDavid amedai kwamba alimsimamia R. Kelly kwa miaka mingi ni tangu akiwa hana lolote hadi kuwa super star, ishu ni kwamba mwaka jana mambo yalibadilika kati ya McDavid na Kelly ni tofauti zilizo sababisha kampuni yao kuvunjika.

Kwa mujibu wa kesi iliyoko mahakamani inadaiwa kwamba waliweka makubaliano kwamba Kelly atamlipa McDavid $1.3 milioni baada ya mfanikio waliyopata kisha kila mtu ashike 50zake.

McDavid anasema licha ya kwamba malipo ilikuwa iwe $40K kila mwezi kwa kipindi cha miezi 18 ajabu ni kwamba MdDavid amedai hajalipwa kitu bado.

Mtandao wa TMZ.com unaripoti kwamba Kelly ameshtakiwa kwa kutomaliza deni na kwamba MCDavid amemkazia kwasababu anamfahamu vizuri kelly, hasa masiaha yake binafsi na wanawake kwa kipindi kischopungua miaka 20.