Jumatatu, 25 Agosti 2014

ONA JINSI LADY JAY DEE ANAVYOMTESA GADNA WAKE


Idadi ya Likizo za Lady Jay Dee kwenda nchi za nje kila mwaka zimemfanya Gadner G. Habash ambae ni mume wake wa ndoa kuchukua hatua ya kupaza sauti na kuvunja ukimya akidai kupatwa na wivu wa mapenzi na hali inayoashiria upweke, hasa Jay Dee anaposafiri peke yake.

Gadner anafunguka kwamba Lady Jay Dee husafiri kila mwaka ndani ya nyakati tofauti na kuspendi muda wake kwa wiki kadhaa akiwa huko nje ya nchi, na kwamba kwake hazitafsiriwi kama safari bali likizo ambazo hujitokeza katika nyakati za ‘Off Season’.

Baada ya kudadisi ili kufahamu kwanini Lady Jay Dee huchagua mwezi wa Ramadhani kila mwaka kusafiri nje ya nchi kwa mapumziko, Gadner alisema,

Yeye mwenyewe kwa kuheshimu mwezi mtukufu wa Ramadhani ambao anaona wateja wake wengine wanakua wamefunga huwa anaona anyamaze tu kuliko kupigizana nao makelele anaona kama ni kitu ambacho sio hekima kutoa maburudani kwa wakati huo.

Katika mazungumzo hayo Gadner anaendelea kusema, Jay Dee huenda Likizo hata nyakati nyingine mfano mwezi Januari ambao ni ‘OFF SEASON’, si kipindi cha msimu saaana wa maburudani na hata Ramadhani ikifika japokuwa hafanyi kazi akaamua akae tu nyumbani kwahiyo ni kwasababu ndio msimu ambao unapungua sana kutokana na aina ya biashara anayoifanya”.

Akitoa mifano Gadner alisema kuwa aliwahi kuongozana na mkewe Jay Dee, (Cape Town) Africa Kusini, ikiwemo kutembelea hifadhi ya Mlima Kilimanjaro, na kudai kuwa mke wake wakati mwingine husafiri hata kwenda China, na Ufaransa, ingawa hupendelea Marekani zaidi kwasababu huko ana ndugu wengi wa familia yao.

Aidha Gadner anakiri kutokuwa na tatizo dhidi ya watu wanaozungumzia sehemu ya maisha binafsi ya ndoa yao hususani vijembe kuhusu kutokuwa na familia (watoto) na Jay Dee, akifafanua kwamba unapokuwa kwenye ‘Spotlight’ si rahisi kuepuka kukutana na hali hiyo.

Mimi sina tatizo kwa kweli kama mtu akizungumza; kibinadamu tumeumbwa hivyo ujue wakati mwingine vinakuja positive wakati mwingine negative basi unakaza roho tu na kuendelea na kazi, havikwepeki ukishakuwa kwenye Spotlight ila tumezoea kidogo maana ni muda mrefu tupo kwenye hii kazi ”, Alisema.


Gadner anaeleza kwa shauku suala la mafanikio ya Lady Jay Dee, kwamba yanakuja kutokana na msukumo wa wapenzi wa mziki wake kwa ujumla, na kudai kwamba mafanikio yake ni mchanganyiko wa vitu vingi, ukiacha kipaji Jay Dee ana bidii kwa hiyo vyote vinampa msukumo mzuri sana wa mafanikio.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni